Machapisho

MAMBO AMBAYO MAMA MJAMZITO HATAKIWI KUYAFANYA NA MAMBO AMBAYO MAMA MJAMZITO ANATAKIWA KUYAFANYA KATIKA KIPINDI CHOTE CHA UJAUZITO WAKE.

Picha
Mwanamke mjamzito, ni mama mtarajiwa pia uwepo wake ni kwa manufaa ya yeye na kiumbe aliye tumboni. Hivyo basi mama mjamzito hatakiwi kujichukulia yeye kama yeye, badala yake ni yeye na ujauzito wake. Katika kipindi chote cha ujauzito, si miezi mitatu ya mwanzo pekee, mjamzito, hatakiwi: • Kuvuta sigara, hatakiwi kunywa pombe, • Kuwa na msongo wa mawazo, • Kuwa mchafu wa mwili, • Kutoa ujauzito (hapa namaanisha kuwa hatakiwi kutumia dawa zozote kali ambazo zinaweza kuhathiri afya yake na ujauzito wake), • Kula vyakula ambavyo kimsingi havina tija kwake yeye na ujauzito zaidi ya kuchangamsha tu kinywa na kujaza tumbo. Anachotakiwa kufanya mama mjamzito: • Kula vizuri kufanya mazoezi na kupumzika, • Kuanza kiliniki ya mama mjamzito katika wiki ya 16 au amechelewa wiki ya 20 • Kuhudhuria  kiliniki ya ujauzito kadiri anavyopangiwa hadi pale atakapojifingua. • Kufuata na kuielewa elimu inayotolewa na wahudumu wa afya katika kliniki ya mjamzito. • Kuzingatia kanuni za ...

NAMNA YA KUMLEA MTOTO KUWA MTOTO MWENYE KIPAJI (GENIUS).

Picha
Ikiwa unastaajabu namna ya kumlea mtoto wako kuwa mtoto mwenye kipaji, unachohitaji ni kuwa na upendo, kuwa na muda, na kujitoa kwa ajili ya mtoto wako.  Wazazi wengi hufikiri kuwa wanahitaji kuwa wajanja sana, lakini hilo sio la lazima. Mtoto wako anahitaji muda wako. Mtoto wako anahitaji uangalizi wako mzazi. Ndani ya miaka kumi ya mwanzo ya maisha ya mtoto wako, atajifunza mambo mengi ambayo hasingeweza kujifunza wakati wowote wa maisha yake, kwani katika kipindi hiki ubongo wake unakuwa unatengeneza mifumo mingi trilioni kwa trilioni. Kila wakati mwanao hutengeneza kitu kipya, ubongo hufanya mfumo mpya mwingine. Na mifumo hiyo humfanya mwanao kujifunza zaidi katika maeneo mengine. UTAMFANYAJE MWANAO KUWA MWENYE KIPAJI  (GENIUS)? 1. ZUNGUMZA NAYE KWA UFUNDI. Muulize mtoto wako maswali yenye majibu ya kujieleza badala ya kumuuliza maswali yenye majibu ya NDIYO-HAPANA; hii inaweza kumsaidia mtoto kufikiri kuhusu yale anayoyafahamu. Mwache mwanao afaham...

MBINU ZA KUZITUMIA KUCHAGUA JINSIA YA MTOTO UNAYETAKA KUMZAA

Picha
Mzunguko wa Hedhi: Mzunguko wa kawaida wa hedhi kwa wanawake walio wengi ni siku 28. Baadhi ni siku 30, 32, 35. Hii ina maana gani?  Kila baada ya siku 28 mwanamke huyu mwenye mzunguko wake wa hedhi siku 28 ataingia kwenye siku zake. Siku hizi hudumu kwa siku 3 hadi 5 na wengine huenda hadi siku 7.  Na kila siku ya 14 tangu aanze siku zake, yai la kike hutotewa ili kukutana na mbegu ya kiume ili kupata ujauzito, ( yaani kama atakutana na mwenzi wake kwa kipindi cha karibuni ). Ufuatao hapo chini ni Mpangilio wa Mzunguko wa Hedhi kwa Mwanamke Anayeingia Hedhi kila Baada ya Siku 28. 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10,  11, 12, 13,  14  15, 16, 17, 18, 19, 20, 21, 22, 23, 24, 25, 26, 27, 28 √ Siku 1 hadi 7 ni zile siku ambazo mwanamke wa kawaida anaingia blidi. √ Siku 8 hadi 10 ni siku salama hakuna ujauzito. √ Siku ya 11 hadi siku ya 17 ni siku za hatari. Kuna uwezekano wa kupata ujauzito siku hizi. √ Siku ya 14 tangu mwanamke aanze kublidi ndiyo siku...

HAUPO PEKE YAKO. KUPATA UJAUZITO KUNAHITAJI MUDA.

Picha
Hivyo usiwe na wasiwasi na wala usikate tamaa hata kama umekwisha jaribu kupata mimba kwa miezi kadhaa, pasipo mafanikio - hii ni kawaida. Ebu jaribu kufanya hivi:- chukua sarafu ya shilingi mia mbili au shilingi mia moja, kisha irushe juu hadi pale sarafu yako itakapoonekana kwenye upande wa kichwa. Je, umejaribu kuirusha mara ngapi bila kuona upande wa kichwa wa sarafu yako? Endelea kufanya jaribio hilo. Umejaribu mara mgapi? Mara Mbili? Mara tatu? Mara Nne? Mara Tano au zaidi? Kwakuwa uwezekano wa kuirusha sarafu ni asilimia 50 yaani ni mara mbili ya uwezekano wa wewe kupata ujauzito kila mwezi ambao ni asilimia 25, kama itakuchukua mara nne kuirusha sarafu na kisha kuona kichwa, hiyo ni sawa na kujaribu miezi 8 kupata ujauzito kisha ukafanikiwa kupata ujauzito. Hivyo, endapo umejaribu kupata ujauzito kwa miezi minne mfululizo au zaidi, usikate tamaa. Haupo peke yako. Kuna mamilioni ya wanandoa wanaojaribu kupata mimba kwa kiwango hicho hicho ulichojaribu wewe pasipo mafa...

Ukweli Kuhusu Kemikali Chumvi Sodium Nitrate/Nitrite

 Kemikali chumvi na viambata (ingredients) vinavyotumika kuhifadhia vyakula vya viwandani: • Sodium nitrate (NaNO3) na Sodium nitrite (NaNO2) ni kemikali chumvi zinazoongezwa kwenye vyakula kama soseji (hot dogs), nyama za nguruwe (bacon) na bidhaa nyingine za nyama kuzisaidia zisiharibike na kuzisaidia ziendelee kubaki na rangi yake ile ya pinki, pia husaidia kuhifadhi zisishambuliwe na bakteria waharibifu (crostridium botulinum) • Kiwango kikubwa cha Nitrate/nitrite hutumika pia kupulizia kwenye udongo mashambani kuua wadudu wanaoharibu mazao, kemikali hii huweza kuwepo kwenye mazao ya shambani. • Kemikali chumvi za Nitrate/nitrite zinaongeza hatari ya mtu kupata saratani kwa watu wote, watoto wadogo na hata watu wazima. Shirika la Afya Duniani (WHO) linatoa onyo kuwa kemiali chumvi za Nitrate/nitrite hupelekea mtu kupata saratani ya ubongo, saratani ya tumbo na utumbo, Saratani ya chembe hai za damu (leukemia) pamoja na saratani ya Pua na Koo. Ili kuepukana na haya, ni vem...

MITINDO YA MAISHA INAVYOATHIRI AFYA YA UZAZI

Picha
MAMBO 11 AMBAYO MWANAMKE HATAKIWI KUYAFANYA KWENYE UKE WAKE. Ni muhimu kuufahamu mwili wako. Hasa hasa sehemu zako za siri. Sehemu za siri za mwanamke ni tata sana kutokana na heshima yake. Mwanamke akiweza kutunza uke wake ni jambo la maana zaidi kwa afya yake. Yafuatayo ni mambo 11 ambayo mwanamke hatakiwi kufanya kwenye uke wake; #1. USIPAKE VITU VITAMU UKENI: Baadhi ya wanawake husema kuwa kuweka sukari au asali ukeni kunaongeza ladha ya tendo la ndoa kwa mwanaume. Usifanye hivyo! Kwasababu uke unajisafisha wenyewe, hivyo kuweka sukari au asali ukeni kunaharibu Uwiano sahihi wa nyongo na tindikali ( pH balance ) uliopo ukeni hali itakayopelekea kupata maambukizi ya kuvu ukeni ( fangasi ukeni ). #2. USITUMIE MAJI YA JOTO AU YA BARIDI SANA KUSAFISHA UKENI: Wakati wa kuoga hakikisha, ukeni usitumie maji ya joto sana. Kutapelekea kukauka hatimaye michubuko. Maji ya uvuguvugu yanafaa. #3. MAPAMBO : Usiweke mapambo ya aina yoyote ukeni. #4. EPUKA KUVAA NGUO ZA KUBAN...

Utakavyoishi bila ya kuwa na sehemu za siri (Private parts)

Picha
Photo credit:Mediscape Watu wanaweza kuwa na uume, wanaweza kuwa na uuke na viungo vingine vya uzazi na bado vikawa si vya lazima kwao. Kwa mfano, ili kutibu aina fulani ya saratani kwa wanaume, wanaume hao hulazimika kuondolewa korodani, au kwa wanawake, wanawake hao hulazimika kuondolewa kizazi (uterus). Na kuna wanawake ambao wamezaliwa wakiwa hawana baadhi ya sehemu kwenye mifumo yao ya uzazi, ikiwemo sehemu zao za uke. Mwanamke mmoja mwenye ugonjwa nadra sana unaoitwa "Mayer-Rokitansky-Kuster-Hauser syndrome" aliandika kwenye mtandao wa Cosmopolitan kwamba, alizaliwa bila kuwa na kizazi au theluthi mbili (2/3) ya uke wake. Mwanamke huyo anaelezea kwamba yeye hawezi kuingia kwenye siku zake za mwezi, na hivyo hawezi kupata ujauzito, lakini bado ana mzunguko wake wa vichocheo (hormonal cycle) — “Mimi sina kizazi (uterus) na wala siingii kwenye hedhi kila mwezi. ...Ninataga mayai ya uzazi (ovulation) kila mwezi, lakini badala ya mayai hayo ya uzazi kusafiri ku...