MAMBO AMBAYO MAMA MJAMZITO HATAKIWI KUYAFANYA NA MAMBO AMBAYO MAMA MJAMZITO ANATAKIWA KUYAFANYA KATIKA KIPINDI CHOTE CHA UJAUZITO WAKE.

Mwanamke mjamzito, ni mama mtarajiwa pia uwepo wake ni kwa manufaa ya yeye na kiumbe aliye tumboni.

Hivyo basi mama mjamzito hatakiwi kujichukulia yeye kama yeye, badala yake ni yeye na ujauzito wake.

Katika kipindi chote cha ujauzito, si miezi mitatu ya mwanzo pekee, mjamzito, hatakiwi:
• Kuvuta sigara,
hatakiwi kunywa pombe,
• Kuwa na msongo wa mawazo,
• Kuwa mchafu wa mwili,
• Kutoa ujauzito (hapa namaanisha kuwa hatakiwi kutumia dawa zozote kali ambazo zinaweza kuhathiri afya yake na ujauzito wake),
• Kula vyakula ambavyo kimsingi havina tija kwake yeye na ujauzito zaidi ya kuchangamsha tu kinywa na kujaza tumbo.

Anachotakiwa kufanya mama mjamzito:
• Kula vizuri kufanya mazoezi na kupumzika,
• Kuanza kiliniki ya mama mjamzito katika wiki ya 16 au amechelewa wiki ya 20
• Kuhudhuria  kiliniki ya ujauzito kadiri anavyopangiwa hadi pale atakapojifingua.
• Kufuata na kuielewa elimu inayotolewa na wahudumu wa afya katika kliniki ya mjamzito.
• Kuzingatia kanuni za afya, kwa kuwa msafi kimwili, kunywa maji safi na salama.
• Kuepuka kuzini.
• Kupata uchunguzi na matibabu ya magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza mapema.
• Kufurahia tendo la ndoa na mume wake.
• Kufanya maandalizi ya uzazi salama na malezi bora ya mtoto atakayezaliwa  kwa manufaa ya familia na taifa kwa ujumla.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBINU ZA KUZITUMIA KUCHAGUA JINSIA YA MTOTO UNAYETAKA KUMZAA

MITINDO YA MAISHA INAVYOATHIRI AFYA YA UZAZI