MITINDO YA MAISHA INAVYOATHIRI AFYA YA UZAZI

MAMBO 11 AMBAYO MWANAMKE HATAKIWI KUYAFANYA KWENYE UKE WAKE.

Ni muhimu kuufahamu mwili wako. Hasa hasa sehemu zako za siri.
Sehemu za siri za mwanamke ni tata sana kutokana na heshima yake. Mwanamke akiweza kutunza uke wake ni jambo la maana zaidi kwa afya yake.

Yafuatayo ni mambo 11 ambayo mwanamke hatakiwi kufanya kwenye uke wake;

#1. USIPAKE VITU VITAMU UKENI:

Baadhi ya wanawake husema kuwa kuweka sukari au asali ukeni kunaongeza ladha ya tendo la ndoa kwa mwanaume. Usifanye hivyo!

Kwasababu uke unajisafisha wenyewe, hivyo kuweka sukari au asali ukeni kunaharibu Uwiano sahihi wa nyongo na tindikali ( pH balance ) uliopo ukeni hali itakayopelekea kupata maambukizi ya kuvu ukeni ( fangasi ukeni ).

#2. USITUMIE MAJI YA JOTO AU YA BARIDI SANA KUSAFISHA UKENI:

Wakati wa kuoga hakikisha, ukeni usitumie maji ya joto sana. Kutapelekea kukauka hatimaye michubuko. Maji ya uvuguvugu yanafaa.

#3. MAPAMBO :
Usiweke mapambo ya aina yoyote ukeni.

#4. EPUKA KUVAA NGUO ZA KUBANA:

Kila mwanamke ana angalau pea moja ya suruali ya kubana ( skinny jeans ) kwenye kabati lake la nguo.

Lakini sidhani kama kuna anayefahamu kuwa nguo za kubana zinaumiza uke wake.
"Kila kitu ni kizuri tu kwa kiasi kikizidi ni tatizo"" (Everything is only good in moderation,) anasema Dr. Ava Shamban, daktari wa magonjwa ya wanawake.

" “Nguo za kubana zinapovaliwa mara kwa mara zina madhara kama vile kuvu ukeni ( fangasi ) au magonjwa mengine ya ngozi yanayotokana na mgandamizo ( kitaalamu huitwa "Pressure acne"").

Ni vigumu kuacha kuvaa nguo za kubana lakini epuka kuvaa mara kwa mara.

#5. UCHAFU:
Wanawake wengi hutumia uume wa midoli kama njia mojawapo ya kujifikisha kileleni. Lakini siku zote hakikisha unasafisha chochote unachokiingiza ukeni. Hata kama ni kidole chako mwenyewe.

# 6: USITUMIE VILAINISHO UKENI:

#7. USITUMIE SABUNI ZA MARASHI UKENI:

 Wanawake wengi wana harufu mbaya ukeni, hivyo hutumia sabuni za marashi wakidhani kuwa kufanya hivyo ni kumaliza tatizo.

Kusafisha uke kwa kutumia sabuni za marashi kunapelekea maambukizi na michubuko kutokana na kemikali zilizopo kwenye sabuni hizo.

Harufu mbaya ukeni mara nyingi hutokana na vyakula unavyokula.

#8. USIJIPULIZIE MARASHI UKENI:

#9. USIJITIE VIDOLE UKENI KWA LENGO LA KUJISAFISHA: (DOUCHING)
Uke unajisafisha wenyewe.

#10. USIJIKUNE:

Ingawa kuna wakati uke unawasha, lakini usijaribu kujikuna.
Unaweza kupata mchubuko.

Sababu zinazopelekea kujikuna ukeni ni pamoja na maambukizi ya bakteria ukeni ( bacterial vaginosa ), kuvu wa ukeni, ( fangasi ), na magonjwa mengine ya ngozi.

11. USITUMIE GUGO (GOOGLE) KUJITIBU MAGONJWA YA UKENI:
Siku hizi watu wengi hupenda kujitibu wenyewe kwa kutumia Gugo.
Usifanye hivyo! Nenda kwa daktari kapate tiba na ushauri wa kitaalamu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBINU ZA KUZITUMIA KUCHAGUA JINSIA YA MTOTO UNAYETAKA KUMZAA