HAUPO PEKE YAKO. KUPATA UJAUZITO KUNAHITAJI MUDA.
Hivyo usiwe na wasiwasi na wala usikate tamaa hata kama umekwisha jaribu kupata mimba kwa miezi kadhaa, pasipo mafanikio - hii ni kawaida.
Ebu jaribu kufanya hivi:- chukua sarafu ya shilingi mia mbili au shilingi mia moja, kisha irushe juu hadi pale sarafu yako itakapoonekana kwenye upande wa kichwa. Je, umejaribu kuirusha mara ngapi bila kuona upande wa kichwa wa sarafu yako?
Endelea kufanya jaribio hilo. Umejaribu mara mgapi? Mara Mbili? Mara tatu? Mara Nne? Mara Tano au zaidi?
Kwakuwa uwezekano wa kuirusha sarafu ni asilimia 50 yaani ni mara mbili ya uwezekano wa wewe kupata ujauzito kila mwezi ambao ni asilimia 25, kama itakuchukua mara nne kuirusha sarafu na kisha kuona kichwa, hiyo ni sawa na kujaribu miezi 8 kupata ujauzito kisha ukafanikiwa kupata ujauzito.
Hivyo, endapo umejaribu kupata ujauzito kwa miezi minne mfululizo au zaidi, usikate tamaa. Haupo peke yako. Kuna mamilioni ya wanandoa wanaojaribu kupata mimba kwa kiwango hicho hicho ulichojaribu wewe pasipo mafanikio.
Tafiti za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema kuwa tangu mwaka 1990 hadi mwaka 2010 kwa miaka 10 mfululizo idadi ile ile ya wanandoa milioni 48.5 waliojaribu kupata mtoto hawakuweza kupata mtoto.
Kati ya wanandoa wanne wanaojaribu kupata mtoto ni mwanandoa mmoja tu ndiye hupata mtoto duniani.
Mara nyingi kupata ujauzito ni kama, mchezo wa bahati nasibu.
Kwa bahati njema, kuna mambo mnayoweza kuyafanya kama wanandoa kuongeza uwezekano wenu wa kupata mimba kila mwezi.

Maoni
Chapisha Maoni