Utakavyoishi bila ya kuwa na sehemu za siri (Private parts)
![]() |
| Photo credit:Mediscape |
Watu wanaweza kuwa na uume, wanaweza kuwa na uuke na viungo vingine vya uzazi na bado vikawa si vya lazima kwao.
Kwa mfano, ili kutibu aina fulani ya saratani kwa wanaume, wanaume hao hulazimika kuondolewa korodani, au kwa wanawake, wanawake hao hulazimika kuondolewa kizazi (uterus).
Na kuna wanawake ambao wamezaliwa wakiwa hawana baadhi ya sehemu kwenye mifumo yao ya uzazi, ikiwemo sehemu zao za uke.
Mwanamke mmoja mwenye ugonjwa nadra sana unaoitwa "Mayer-Rokitansky-Kuster-Hauser syndrome" aliandika kwenye mtandao wa Cosmopolitan kwamba, alizaliwa bila kuwa na kizazi au theluthi mbili (2/3) ya uke wake.
Mwanamke huyo anaelezea kwamba yeye hawezi kuingia kwenye siku zake za mwezi, na hivyo hawezi kupata ujauzito, lakini bado ana mzunguko wake wa vichocheo (hormonal cycle) — “Mimi sina kizazi (uterus) na wala siingii kwenye hedhi kila mwezi. ...Ninataga mayai ya uzazi (ovulation) kila mwezi, lakini badala ya mayai hayo ya uzazi kusafiri kupitia mirija ya falopia (falopian tubes), mayai hayo uharibika baada ya kutagwa na kokwa zangu za uzazi (ovaries).”
Mwanaume mmoja alizaliwa bila kuwa na uume, kwa mujibu wa mtandao wa Independent, mwanaume huyo anaishi sehemu kubwa ya maisha yake kawaida kabisa na bado amependa wanawake wengi na kushiriki nao ngono kwa namna nyingine tofauti ile iliyozoeleka.

Maoni
Chapisha Maoni