NAMNA YA KUMLEA MTOTO KUWA MTOTO MWENYE KIPAJI (GENIUS).


Ikiwa unastaajabu namna ya kumlea mtoto wako kuwa mtoto mwenye kipaji, unachohitaji ni kuwa na upendo, kuwa na muda, na kujitoa kwa ajili ya mtoto wako. 

Wazazi wengi hufikiri kuwa wanahitaji kuwa wajanja sana, lakini hilo sio la lazima. Mtoto wako anahitaji muda wako. Mtoto wako anahitaji uangalizi wako mzazi.

Ndani ya miaka kumi ya mwanzo ya maisha ya mtoto wako, atajifunza mambo mengi ambayo hasingeweza kujifunza wakati wowote wa maisha yake, kwani katika kipindi hiki ubongo wake unakuwa unatengeneza mifumo mingi trilioni kwa trilioni. Kila wakati mwanao hutengeneza kitu kipya, ubongo hufanya mfumo mpya mwingine. Na mifumo hiyo humfanya mwanao kujifunza zaidi katika maeneo mengine.

UTAMFANYAJE MWANAO KUWA MWENYE KIPAJI  (GENIUS)?

1. ZUNGUMZA NAYE KWA UFUNDI.
Muulize mtoto wako maswali yenye majibu ya kujieleza badala ya kumuuliza maswali yenye majibu ya NDIYO-HAPANA; hii inaweza kumsaidia mtoto kufikiri kuhusu yale anayoyafahamu.
Mwache mwanao afahamu kuwa unaheshimu na unathamini mawazo yake. Pia, unapokuwa unazungumza na mwanao, usijaribu kuzungumza naye kwa kutumia "lugha ya kitoto" (childish language) bali tumia maneno uliyoyazoea. Hii itamsaidia mtoto kuboresha msamiati na kumfanya afahamu lugha. Anaweza hasipate maana ya misamiati hiyo mwanzoni, lakini atapata maana hapo baadaye kadili atakavyokuwa anakutana nayo katika kukua kwake.

2. MSOMEE MWANAO.
Kumsomea mwanao humsaidia ubongo wake kufanya muunganiko wa matukio anayokutana nayo katika mazingira yanayomzunguka na kumpa taarifa mbalimbali kuhusu ulimwengu na maisha. Ni ukweli ulio wazi kwamba kumsomea mwanao mapema kunaweza kumfanya kuwa mjanja na kumrahisishia kujifunza. Wataalamu wanaamini kuwa kusoma ni msingi wa maarifa. Pia unaweza kushiriki mara kwa mara kusomeana na mtoto, hali itakayomsaidia kunufaika kutokana na maongezi haya kwa kumuongezea uwezo wa kufikiri na kujieleza mbele za watu pia.

3. MPE SIFA ZA WASTANI.
Sifa zilimfanya sifa afanye sifa zisizo na maarifa.
Kumsifu sana mtoto wako anapofanya mambo mazuri kunamfanya ajione kuwa yeye ni wajuu zaidi. Hali itakayompelekea apate msongo. Badala yake mpe sifa za wastani pale anapofanya vizuri au hata pale anapopata matokeo yasiyoridhisha kwenye mitihani yake. Mwambie "Umefanya vizuri" Kumpongeza anapofanya vibaya au anapofanya vizuri ni muhimu katika maisha yake ya kujifunza.

4. MTIE MOYO, MPE MATUMAINI.
Watoto wakiwa katika umri mdogo kabla hawajaanza shule, huwa ni wadadisi (curiosity) wa kutaka kufahamu karibu kila kitu kilichopo katika mazingira yanayowazunguka. Mara tu wanapofikisha umri wa kuanza shule, ile tamaa au shahuku ya udadisi wa kutaka kufahamu mambo mengi katika maeneo yanayowazunguka inapungua au inapotea kabisa. Kama mzazi jaribu kufanya mambo ambayo yatarudisha ile hali ya kuwa na tamaa ya kutaka kufahamu mambo mengi zaidi kwa mtoto wako, lakini katika mtindo wa utu uzima na sio kiutoto utoto tena. Mpeleke kwenye sanaa za michoro ya picha (art galleries) ajionee, mpeleke kwenye maonesho ya muziki ajionee, mpeleke kwenye makumbusho/makavazi (museums) ajionee, mpeleke pia hata kwenye maktaba, huko ataweza kujifunza mambo mapya ambayo yanaweza kukuvutia wewe na yeye pia.

5. KAMATIA KILA FURSA KUMFUNDISHA MWANAO.
Unaporudi nyumbani kutoka kazini, zungumza na mtoto wako kuhusu ulichokifanya ukiwa kazini. Vile vile unaweza kumchukua na kwenda naye kufanya manunuzi (shopping) na muoneshe namna ya kuchagua na kulinganisha bei za bidhaa na ubora wa bidhaa kwa majina ya bidhaa husika. Kuna fursa za kutosha kumfundisha mtoto wako kuihusu dunia na maisha ya kila siku duniani.!

©Afyaswahili 2017

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBINU ZA KUZITUMIA KUCHAGUA JINSIA YA MTOTO UNAYETAKA KUMZAA

MITINDO YA MAISHA INAVYOATHIRI AFYA YA UZAZI