Ukweli Kuhusu Kemikali Chumvi Sodium Nitrate/Nitrite

 Kemikali chumvi na viambata (ingredients) vinavyotumika kuhifadhia vyakula vya viwandani:

• Sodium nitrate (NaNO3) na Sodium nitrite (NaNO2) ni kemikali chumvi zinazoongezwa kwenye vyakula kama soseji (hot dogs), nyama za nguruwe (bacon) na bidhaa nyingine za nyama kuzisaidia zisiharibike na kuzisaidia ziendelee kubaki na rangi yake ile ya pinki, pia husaidia kuhifadhi zisishambuliwe na bakteria waharibifu (crostridium botulinum)

• Kiwango kikubwa cha Nitrate/nitrite hutumika pia kupulizia kwenye udongo mashambani kuua wadudu wanaoharibu mazao, kemikali hii huweza kuwepo kwenye mazao ya shambani.

• Kemikali chumvi za Nitrate/nitrite zinaongeza hatari ya mtu kupata saratani kwa watu wote, watoto wadogo na hata watu wazima. Shirika la Afya Duniani (WHO) linatoa onyo kuwa kemiali chumvi za Nitrate/nitrite hupelekea mtu kupata saratani ya ubongo, saratani ya tumbo na utumbo, Saratani ya chembe hai za damu (leukemia) pamoja na saratani ya Pua na Koo. Ili kuepukana na haya, ni vema ukaacha kutumia kemikali chumvi za Sodium Nitrate/nitrite.

• Kemikali chumvi za Nitrate/nitrite zinaathiri mzunguko wa damu, hasa kwa watoto wadogo wanaweza kupata tatizo linalofahamika kwa kizungu kama "Blue baby syndrome". Hali hii hutokea pale kemikali chumvi za nitrate/nitrite zinapoungana na chembe hai nyekundu za damu, na kuharibu uwezo wa chembe hai za damu kusafirisha oksijeni (uhai) kwenda sehemu mbalimbali za mwili.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBINU ZA KUZITUMIA KUCHAGUA JINSIA YA MTOTO UNAYETAKA KUMZAA

MITINDO YA MAISHA INAVYOATHIRI AFYA YA UZAZI