Dawa za kuzuia mimba na hatari ya kupata saratani ya matiti

Matumizi ya dawa za homoni kwa ajili ya kuzuia mimba (hormonal contraceptives) zinamuongezea mwanamke hatari ya kupata saratani ya matiti kwa asilimia 38%, kutegemea na muda atakaokuwa ametumia dawa hizo., tafiti zimebainisha.



Hatari hiyo inahusisha wanawake wote wanaotumia dawa za vidonge (pills), sindano (injections) na vitanzi (IUCDs) -- ukilinganisha na wanawake ambao hawajawahi kabisa kutumia dawa hizo.
Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Copenhagen (University of Copenhagen) walihusisha wanawake chini ya miaka 50 wapatao milioni 1.8 nchini Denmark na walikuwa wakiwafuatilia wanawake hao kwa miaka 11.
Matokeo ya tafiti hiyo ya miaka 11 yalichapishwa Jumatano hii kwenye jarida la New England Journal of Medicine la nchini Uingereza kama ifuatayo:-
Wanawake waliotumia dawa za vidonge, sindano au kitanzi kuzuia mimba, kwa muda wa chini ya mwaka 1 wana hatari ya kupata saratani ya matiti kwa asilimia 9% , na waliotumia dawa hizo kwa muda wa miaka zaidi ya 10 wana hatari ya kupata saratani ya matiti kwa asilimia 38%.
Saratani ya matiti ni mara chache huwapata wanawake wenye umri mdogo chini ya miaka 35.

Dalili za Saratani ya Matiti.
Moja ya mabadiliko yafuatayo kwenye matiti yanaweza kuwa ni dalili za saratani ya matiti:
- Uvimbe kwenye matiti au sehemu ya matiti kuwasha.
- Maumivu kwenye matiti, au chuchu au chuchu kuzama ndani.
- Wekundu, magamba au kuongezeka unene kwa chuchu au ngozi ya titi au matiti.
- Titi kutoa majimaji tofauti na maziwa.
- Uvimbe maeneo ya kwenye kwapa.

Mabadiliko haya yanaweza kuwa pia ni ishara za matatizo mengine ya kawaida tofauti na saratani ya matiti, kama vile maambukizi ya bakteria kwenye matiti, au vivimbe maji (cyst).
Ni muhimu kumuona daktari punde tu unapogundua mabadiliko yoyote kwenye matiti yako.
Saratani ya matiti ni saratani inayowapata wanawake, ambapo zaidi ya watu milioni 1.7 duniani wanaugua saratani ya matiti.
Ubelgiji ndio nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na watu wengi wanaogua saratani ya matiti ikifuatiwa na nchi ya Denmark na Ufaransa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBINU ZA KUZITUMIA KUCHAGUA JINSIA YA MTOTO UNAYETAKA KUMZAA

MITINDO YA MAISHA INAVYOATHIRI AFYA YA UZAZI