Jifunze Jinsi Ulimi Wako Unavyoweza Kukuambia Hali ya Afya Yako.
Je, unafahamu kuwa ulimi wako unaweza kukuambia mengi kuhusu afya yako?. Jichunguze, simama mbele ya kioo, toa ulimi wako nje na uuchunguze rangi yake.Ulimi kama kilivyo kiungo kingine, kinasaidia kuzungumza, kuonja, kumeza.
1. Ulimi wako ni wa pinki na mororo.?
Ulimi wako ukiwa mororo na hauna vidoti doti, ukiwa na rangi ya udhurungi (pinki) na usiopoteza ladha, hiyo ni ishara kuwa mwili wako una afya njema.
2. Ulimi wako unaonekana mwekundu kama mnofu wa nyama?
Hii ni ishara ya upungufu wa vitamini mwilini unaosababishwa na kutokula mlo kamili. Unaweza ukakosa vitamini B 12 na vitamini B 9 (folic acid). Unashauriwa kula mboga mboga za majani kwa wingi ili kurejesha afya yako na kufanya muonekano mzuri wa ulimi wako.
3. Je, ulimi wako umepasuka pasuka?
Hali hii ya kupasuka pasuka kwa ulimi hutokana na hali ya kinga za mwili kuzishambulia chembe hai muhimu za mwili (kitaalam hufahamika kama "autoimmune disorder).
Pia mara nyingi hali kama hii huwa ni ya kawaida, na huwapata watoto wadogo. Unapoona hali kama hii onana na daktari wako wa kinywa na meno (dentist) haraka iwezekanavyo.
4. Je, Ulimi wako una utando mweusi?
Mara nyingi ni kutokana na uchafu wa kinywa na meno. Utando mweusi ulimini pia inaweza kuonekana kwa watu wenye kisukari.
Wagonjwa wanaotumia dawa za kutibu saratani au wanaotumia dawa za kuua viini (antibiotics) nao pia huwa na utando wa kahawia kwenye ulimi.
Safisha meno na kinywa chako vizuri ili kuzuia viini kuzaliana.
5. Je, Ulimi wako una utando mweupe?
Ulimi wako ukionekana hivi, onana na daktari wako haraka iwezekanavyo. Utando mweupe juu ya ulimi ni kielelezo kwamba fangasi wamezaliana kwenye ulimi wako. Watu wenye kinga dhaifu ya mwili, au watu wanaovuta sigara, utando mweupe kwenye ulimi ni ishara ya hatari ya saratani.





Mm nimetokewa na hali kama no 5 ila ninamsongo wa mawazo ya muda mrefu na nitafanyeje hii ali iishe jamani ushauri
JibuFuta